Home Page Towns & Cities Events & Up Coming Events Maps Of Tanzania Contact Us


Headlines
Foreign News
Mon News
Tues News
Wed News
Thurs News
Fri News
Sat News
Horoscopes
Cartoon



Tanzanian Art Once there was a man called Eduardo S. Tingatinga.

Established in 1960s
Today, "Tingatinga" is the Tanzanian term for this form of art, known mostly around the world.

Tourism In Tanzania
Tanzania Tourist Board
IPS Building, Azikiwe Street .... PO BOX: 2485, Dar es Salaam Phone: 255 22 2111244/5

Tanzania Private Sector
Tanzania Private Sector Foundation
TPSF PO BOX: 11313, D.S.M Phone: 255 22 2129433

Looking to Invest In Tanzania
Tanzania Investment Centre
PO BOX: 938, Dar es Salaam Phone: 255 22 2116328-32 Fax: 255 22 2118253

 

 

You are here > News > Monday News

your one stop travel shop

Last Updated:16.08.2010

ENGLISH | SWAHILI | SPORTS

 

Simba yahama Zenji, Echesa amvuruga Phiri

KIUNGO tegemeo wa Simba Mkenya, Hillary Echessa ameumia mazoezini kwenye Uwanja wa ngome mjini Zanzibar, lakini timu hiyo inahama kambi kuepuka fitna za Yanga.

Echessa akicheza kwenye nafasi ya kiungo na Mohammed Banka msimu uliopita waliifanya Simba tishio na haikupoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kutoa sare mbili rekodi ambayo Kocha Patrick Phiri anajivunia na kuiboresha zaidi msimu huu lakini mambo yameharibika.

Phiri aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa mchana kwenye kambi ya Simba mjini Zanzibar kuwa watashinda mechi ya Jumatano dhidi ya Yanga, lakini Echessa ameumia na atakuwa nje kwa kipindi kisichopungua miezi miwili na itawagharimu.

"Echessa amefanyiwa uchunguzi kwa mionzi leo(jana Ijumaa) imebainika kuwa amejitonesha lile goti lililokuwa linamsumbua na itabidi akae nje ya Uwanja kwa kipindi ambacho hakitapungua miezi miwili,"alisema Phiri akionekana asiye na furaha.

"Kuumia kwake ni pengo kubwa kwavile ni tegemeo katika mfumo wangu haswa wakati kama huu ambao tuna mechi ngumu ya watani wa jadi na ligi iko karibu kuanza.

"Wapo wachezaji kama Nico Nyagawa na Patrick Ochan ambao wanaweza kuziba nafasi yake lakini kumkosa mchezaji muhimu kama Echessa ni tatizo kubwa haswa ukizingatia kwamba kipa namba moja Juma Kaseja tayari ni majeruhi na atakuwa nje ya Uwanja kwa muda.

"Namuamini sana kipa wangu Ally Mustapha na nimemwambia huu ndio wakati wa kuonyesha uwezo wake na kuvaa vilivyo viatu vya Kaseja, ni kipa mzuri ndio maana nilimsajili kwa mara nyingine. Lakini ukweli upo wazi Kaseja ni kipa bora wa nchi hii kutokana na rekodi aliyoweka msimu uliopita kwa kutopoteza mchezo hata mmoja."

"Lakini kambini morali ya wachezaji hususani hawa wapya ipo juu, kila mmoja anaonyesha juhudi sana, "alisema Phiri na kusisitiza kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa ngao ya hisani Jumatano dhidi ya Yanga na wachezaji wake wamemthibitishia kwamba asiwe na wasiwasi.

Habari toka ndani ya uongozi zinasema kuwa mikakati ilikuwa inaendelea ili kuhakikishia baada ya mazoezi ya jana Ijumaa jioni timu inahama kwenye hosteli za "Kwa Zakaria" eneo la Mbweni na kuhamia sehemu nyingine hukohuko Visiwani na hata Uwanja wa Fuoni watauhama kuanzia leo Jumamosi.

Simba imeona sura zisizo za kawaida Uwanjani na maeneo ya Mbweni na kupata wasiwasi wa hujuma. "Kuhama kambi ni jambo la kawaida inapofika kwenye mechi ya Simba na Yanga, mi sishangai," alisema Phiri huenda akamchezesha Nyagawa badala ya Echessa.

 

Poulsen:Fitna za Simba, Yanga hazisumbui

FITINA za Simba na Yanga sio kitu kigeni kwa Kocha mpya wa Taifa Stars, Jan Borge Poulsen, ambaye amebainisha yuko ngangari kufanya kazi katika mazingira hayo.

Poulsen, ambaye alitua nchini Jumapili iliyopita, aliiambia Mwanaspoti fitina na mizengwe ni sehemu ya siasa za soka na anaelewa upinzania wa jadi wa Simba na Yanga zinazopambana Jumatano ijayo.

Make Comments About this Article click here

 




TANServe © 2008
Privacy Policy Terms Of Use
Main Page     |     City     |     Events     |     Map     |     Tourism     |     Help