Home Page Towns & Cities Events & Up Coming Events Maps Of Tanzania Contact Us


Headlines
Foreign News
Mon News
Tues News
Wed News
Thurs News
Fri News
Sat News
Horoscopes
Cartoon



Tanzanian Art Once there was a man called Eduardo S. Tingatinga.

Established in 1960s
Today, "Tingatinga" is the Tanzanian term for this form of art, known mostly around the world.

Tourism In Tanzania
Tanzania Tourist Board
IPS Building, Azikiwe Street .... PO BOX: 2485, Dar es Salaam Phone: 255 22 2111244/5

Tanzania Private Sector
Tanzania Private Sector Foundation
TPSF PO BOX: 11313, D.S.M Phone: 255 22 2129433

Looking to Invest In Tanzania
Tanzania Investment Centre
PO BOX: 938, Dar es Salaam Phone: 255 22 2116328-32 Fax: 255 22 2118253

 

 

You are here > News > Saturday News

your one stop travel shop

Last Updated: 21.8.2010

ENGLISH | SWAHILI | SPORTS

Uingereza kuendelea kuwa mshirika wa Tanzania -Balozi

UINGEREZA imesema itaendelea kuwa mshirika wa Tanzania katika maendeleo kwa kuwa mazingira yake kisiasa yanavutia uwekezaji.Balozi wa Uingereza nchini, Diane Corner alisema hayo jana jijini Dar es Salaam.Alisema ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ni tulivu, ina rasilimali za kutosha na inavutia kwa uwekezaji.

"Tanzania ni nchi tulivu na mazingira yake yanavutia uwekezaji. Uingereza imeamua kuiweka (Tanzania) katika ramani yake ya uwekezaji," alisema Balozi Corner na kubainisha kuwa mwaka jana, Waingereza 55,000 walitembelea Tanzania kwa ziara za kitalii.

Alisema mbali na utalii huo, takriban Waingereza 7,000 wanaishi nchini kwa shughuli mbalimbali.

Balozi Corner alisifia vyombo vya habari nchini, akisema vimenatoa mchango mkubwa katika kukuza demokrasia.

"Nisingependa kuzungumzia chombo kimoja bali mtazamo wangu kuhusu vyombo vya habari. Kwa kweli vimechangia sana hali hii ya kuwa na demokrasia ya kuridhisha," alisema.

Alisema vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa huru kuliko ilivyokuwa miaka ya tisini na kwamba, sasa watu wanapata habari zaidi.

Awali mkurugenzi wa Mwananchi Communications, Sam Shollei alieleza kuwa anaamini mabadiliko katika siasa za Tanzania, yanaweza kutokea katika chaguzi zijazo kutokana na mabadiliko mbalimbali.

"Nimeanza kuona wimbi la vijana likijiingiza kwenye siasa na wazee wakianguka. Hii inaashiria kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa baada ya Rais Kikwete," alisema Shollei.

Kabla ya kukutana na Shollei na baadaye wahariri wa magazeti yanayochapishwa kampuni hiyo, Balozi Corner alitembelea vitengo mbalimbali, ikiwemo kiwanda cha uchapishaji, ambako alivutiwa na mtambo wa kisasa wa kuchapisha magazeti unaomilikiwa na MCL


Rushwa ilikithiri kura za maoni CCM-Makweta

WAZIRI wa zamani wa serikali ya awamu ya kwanza Jackson Makweta, ambaye ameangushwa kwenye kura za maoni za CCM, amevunja ukimya akisema utaratibu uliotumika kupata wagombea wa CCM ulikithiri kwa rushwa.

Makweta, ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini mkoani Iringa tangu mwaka 1995, pia alisema wengi wa wanachama wa CCM waliopiga kura hawakuwa na uelewa wa kutosha kujua umuhimu wa kura na kwamba wingi huo ulisababisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Makweta, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, alisema hayo juzi katika kipindi maalumu cha mjadala kuhusu mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM kilichorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Mjadala huo ulimjumuhisha Profesa Paramagamba Kabudi, John Lusinde, ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Mtera kwa tiketi ya CCM, na naibu katibu mkuu wa chama tawala nchini Uganda(NRM), Maiki Mukula.

Make Comments About this Article click here




TANServe © 2008
Privacy Policy Terms Of Use
Main Page     |     City     |     Events     |     Map     |     Tourism     |     Help