Home Page Towns & Cities Events & Up Coming Events Maps Of Tanzania Contact Us


Headlines
Foreign News
Mon News
Tues News
Wed News
Thurs News
Fri News
Sat News
Horoscopes
Cartoon



Tanzanian Art Once there was a man called Eduardo S. Tingatinga.

Established in 1960s
Today, "Tingatinga" is the Tanzanian term for this form of art, known mostly around the world.

Tourism In Tanzania
Tanzania Tourist Board
IPS Building, Azikiwe Street .... PO BOX: 2485, Dar es Salaam Phone: 255 22 2111244/5

Tanzania Private Sector
Tanzania Private Sector Foundation
TPSF PO BOX: 11313, D.S.M Phone: 255 22 2129433

Looking to Invest In Tanzania
Tanzania Investment Centre
PO BOX: 938, Dar es Salaam Phone: 255 22 2116328-32 Fax: 255 22 2118253

 

 

You are here > News > Thursday News

your one stop travel shop

Last Updated: 9.9.2010

ENGLISH | SWAHILI | SPORTS

Mpakistan akamatwa kwa kuchana noti ya Sh 5,000

POLISI mkoani Mwanza limemtia mbaroni raia wa Pakistan baada ya kuchana hadharani noti mmoja ya Sh 5,000.

Tukio hilo, lilitokea jana saa 11:45 asubuhi wakati Mpakistani huyo ambaye jina lake tumelihifadhi akiwa miongoni mwa abiria ambao walikuwa uwanja wa ndege Mwanza wakikaguliwa kwa ajili ya kuingia kwenye ndege ili kunza safari ya kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alisema Raia huyo wa Pakistani alitenda kosa hilo hadharani huku akishuhudiwa na abiria wenzake ambao pia walikuwa wakisubiria kusafiri kwa ndege hiyo ya shirika la Precision.

Kamanda Sirro alisema raia huyo wa Pakistani ni mfanyakazi katika shirika la Catholic Refugees Service (CRS) linalojishughulisha na kutoa huduma na misaada kwa wakimbizi.

“Akiwa kama abiria wengine wakati wakiwa katika ukaguzi kwa ajili ya kuingia ndani ya ndege, huyu alitoa noti moja ya Sh 5,000 na kuanza kuichana chana vipande, kwa kitendo hicho abiria waliokuwepo walikasirishwa na kitendo hicho na kutoa taarifa kwa maofisa usalama ambao walikuja na kumkamata,” alieleza.

Alisema baada ya kuzungumza naye kwa kina alionekana kutokuwa na sababu za msingi na hivyo kuamua kumchukulia hatua na walimkabidhi kwa ofisa wa polisi na kufikisha katika kituo ambako waliendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi.

“Tunavyo vipande vya noti ambayo alivichana kama ushahidi, kitendo hiki kinaonyesha dharau kubwa kwa fedha yetu na taifa letu, na kinaonyesha kukosa ukosefu wa heshima.” alifafanua zaidi Kamanda Sirro.


 

Makamba: CCM haing'oi mabango ya mgombea urais

WAKATI Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa akitaka CCM kuacha kutumia mabango ya mgombea urais wa chama hicho yenye picha za Ikulu, chenyewe kimetunisha misuli kikisema hakitaondoa mabango yake kwani hakuna picha za taasisi hiyo nyeti ya nchi.

Mvutano huo umekuja siku moja baada ya Baraza la Vyama vya Siasa, kutaka CCM iache kutumia nyenzo za Ikulu yakiwemo mabango ambayo picha zake zimeandaliwa kwa gharama za Ikulu.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Makamba alifafanua mambo matatu ya msingi kuhusu mabango ya mgombea urais wa chama hicho Jakaya Kikwete.

 

Make Comments About this Article click here




Click Here For TANServe Blog

TANServe © 2008
Privacy Policy Terms Of Use
Main Page     |     City     |     Events     |     Map     |     Tourism     |     Help