Home Page Towns & Cities Events & Up Coming Events Maps Of Tanzania Contact Us


Headlines
Foreign News
Mon News
Tues News
Wed News
Thurs News
Fri News
Sat News
Horoscopes
Cartoon



Tanzanian Art Once there was a man called Eduardo S. Tingatinga.

Established in 1960s
Today, "Tingatinga" is the Tanzanian term for this form of art, known mostly around the world.

Tourism In Tanzania
Tanzania Tourist Board
IPS Building, Azikiwe Street .... PO BOX: 2485, Dar es Salaam Phone: 255 22 2111244/5

Tanzania Private Sector
Tanzania Private Sector Foundation
TPSF PO BOX: 11313, D.S.M Phone: 255 22 2129433

Looking to Invest In Tanzania
Tanzania Investment Centre
PO BOX: 938, Dar es Salaam Phone: 255 22 2116328-32 Fax: 255 22 2118253

 

 

You are here > News > Tuesday News

your one stop travel shop

Last Updated:7.9.2010

ENGLISH | SWAHILI | SPORTS

Lipumba amvaa Hawa Ghasia jimboni kwake

SIKU chache baada ya kuishambulia serikali mbele ya mkuu wa wilaya ya Lindi, Magalula Said Magalula, mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana aliwataka wananchi wamuondoe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi, Hawa Ghasia akidai yeye na chama chake cha CCM wameshindwa kuondoa umasikini.


Prof Lipumba, ambaye mtaalamu wa uchumi, pia alisema CUF wakipewa dhamana ya kuendesha nchi watafuta utaratibu huo wa stakabadhi ghalani unaolalamikiwa na wakulima wa maeneo mengi ili kuwaondolea wananchi kero na kuwapunguzia umasikini.

Akihutubia katika vijiji vya Libobe, Mkunwa na Dihimba, Prof Lipumba alisema ameshtushwa na umasikini unaowakabili wananchi wa jimbo hilo licha ya kuwa na mbunge ambaye ni waziri na akaeleza kuwa hali hiyo inasababishwa na utawala mbovu wa CCM.


Awali wananchi hao walimweleza Lipumba usumbufu wanaoupata hasa katika uuzaji wa korosho wakiutaja utaratibu wa stakabadhi ghalani kuwa ni mbovu. Chini ya utaratibu huo, wakulima huuza mazao yao kwa serikali ambayo hununua kumlipa mkulima fedha za kujikumu wakati wakisubiri mazao yao yauzwe ndio wamaliziwe malipo yao. Lakini muda wa malipo unapofika usumbufu huwa mkubwa.


Wananchi pia walilalamikia uhaba wa maji wakisema kuwa jimbo hilo hutegemea visima vya kuchimbwa ambavyo wakati mwingine hukaukiwa maji.

“Hapa tuna uhaba mkubwa wa maji kwa kuwa huu ni msimu wa kiangazi; visima vyenyewe vinakauka... kuhusu uuzaji wa korosho tunazungushwa mno kupata fedha zetu kutokana na uataratibu wa stakabadhi ghalani,” alisema msoma risala katika kijiji cha Libobe.


Wananchi hao walimponda Waziri Ghasia wakisema kuwa tangu ameingia madarakani ameshindwa kutatua kero zao na wala haonekani eneo hilo.
“Hadi sasa Ghasia hajaanza kampeni huku vijijini. Aliwahi kupita hapa siku moja tu. Kwa kiasi kikubwa hajatekeleza ahadi alizotuahidi,” alisema Yasin Abdallah wa Kijiji cha Mkunwa.


Akijibu risala hiyo, Profesa Lipumba alisema kama watamchagua atafuta utaratibu wa stakabadhi ghalani.
“Haiwezekani mkulima auze korosho zake kwa utaratibu ambao kama kilo moja inauzwa kwa Sh3,000, anapewa Sh 2,000 tu, hizo nyingine anaambiwa kuwa Mungu akipenda atalipwa. Mkinichagua nitaufuta utaratibu huu,” alisema.


Katika jimbo hilo CUF wamemsimamisha Chikamba Wananimuka ambaye atapambana na Hawa Ghasia wa CCM.
Mkazi mmoja wa kijiji hicho, Suleiman Said alisema kuwa wataalamu wa mimea walienda kijijini hapo kuchukua vipimo ili kujua tatizo la minazi inayoshambuliwa na magonjwa, lakini hawajarudi tena.
“Wataalamu walikuja kuichunguza miezi kadhaa iliyopita, lakini hawajariudi tena. Minazi inaendelea kufa kama unavyoona,” alisema.


Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, ugonjwa huo usipodhibitiwa unaweza kuangamiza kabisa zao la minazi.
“Ugonjwa huu uliwahi kutokea Zanzibar wakawahi kuudhibiti, lakini naona hapa hakuna jitihada zozote. Usipodhibitiwa utamaliza minazi yote,” alisema.


Lipumba aliendelea kusisitiza sera za chama chake kuhusu elimu ya bure, afya bure na kupambana na ufisadi pindi atakapoingia madarakani.
Mgombea huyo anaendelea na ziara za kampeni katika mikoa ya Kusini Mashariki inayoonekana kuwa na wafuasi wengi wa CUF.

 


Tanzania kuipiku Marekani kwa Uranium

MRADI wa kuchimba madini ya uranium Mkoa wa Ruvuma utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 1,650 kwa mwaka na hivyo kuifanya Tanzania kuwa kinara wa madini hayo duniani, ilifahamika.

Hatua hiyo hiyo itasababisha kuicha nyuma nchi ya Marekani ambayo kwa sasa inavuna tani 1,560 za madini hayo kwa mwaka na kuwa nchi ya kwanza duniani kwa kazi hiyo.

Make Comments About this Article click here




Click Here For TANServe Blog

TANServe © 2008
Privacy Policy Terms Of Use
Main Page     |     City     |     Events     |     Map     |     Tourism     |     Help