Home Page Towns & Cities Events & Up Coming Events Maps Of Tanzania Contact Us


Headlines
Foreign News
Mon News
Tues News
Wed News
Thurs News
Fri News
Sat News
Horoscopes
Cartoon



Tanzanian Art Once there was a man called Eduardo S. Tingatinga.

Established in 1960s
Today, "Tingatinga" is the Tanzanian term for this form of art, known mostly around the world.

Tourism In Tanzania
Tanzania Tourist Board
IPS Building, Azikiwe Street .... PO BOX: 2485, Dar es Salaam Phone: 255 22 2111244/5

Tanzania Private Sector
Tanzania Private Sector Foundation
TPSF PO BOX: 11313, D.S.M Phone: 255 22 2129433

Looking to Invest In Tanzania
Tanzania Investment Centre
PO BOX: 938, Dar es Salaam Phone: 255 22 2116328-32 Fax: 255 22 2118253

 

 

You are here > News > Wednesday News

your one stop travel shop

Last Updated: 8.9.2010

ENGLISH | SWAHILI | SPORTS

Phiri: Hebu mwacheni Humoud

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuacha kumsakama mchezaji wake Abdulhalim Humoud kwa kuwa bado hajazoea mfumo wa timu hiyo.

Phiri alimtetea mchezaji huyo ambaye mwishoni mwa wiki alishindwa kuonyesha cheche zake na badala yake alijikuta akiboronga uwanjani kitendo ambacho kilimfanya kocha huyo raia wa Zambia kumuondoa mapema na kumuingiza Jerry Santo.

Kufuatilia hali hiyo, Humoud alijikuta kwenye wakati mgumu kutoka kwa mashabiki ambao walimtusi na kumtolea maneno ya kejeli, huku wengine wakimzomea na kumdhihaki kwa kuachwa kwake timu ya taifa kitendo ambacho kilimpandisha jazba ambayo alishindwa kujizuia na kuanza kujibu mashambulizi kwa kutoa na yeye lugha chafu kwa mashabiki.

Mchezaji huyo nusura azikunje na mmoja wa mashabiki, lakini aliamuliwa na wachezaji wenzake, huku akizomewa na mashabiki.

Katika mchezo huo wa Simba na Gor Mahia ulichezwa kwenye uwanja wa taifa, Simba ilipokea kipigo cha mabao 3-1 kitu ambacho kilipelekea Mzambia huyo kubadilisha karibu kikosi chote ili kukabilina na wekenya hao.

Lakini Phiri alimtetea Humoud na kusema "ni mchezaji mzuri sana tatizo ni huu mfumo wetu hajauzoea, unajua kila timu ina mfumo wake, mpeni muda taratibu atazoeana.

Simba yaifuata Azam, Yanga kujinoa na AFC Leopard

BAADA ya wiki mbili za mapumziko kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya timu ya taifa 'Taifa Stars' dhidi ya Algeria wachezaji wa Azam, Simba na Yanga mwishoni mwa wiki wanarejea upya kwenye mikiki ya Ligi Kuu Tanzania bara.

Mabingwa watetezi Simba iliondoka jijini Dar es Salaam jana kuelekea Tanga watapokuwa na kibarua kigumu dhidi ya ndugu zao Azam FC wenye malengo ya kutaka kutwaa ubingwa msimu huu.

Huku washindi wa pili wa msimu uliopita Yanga leo watakuwa safarini kuelekea Arusha tayari kwa kuivaa AFC Leopard ya Kenya kabla mchezo wa ligi dhidi AFC Arusha ya huko.

Make Comments About this Article click here




TANServe © 2008
Privacy Policy Terms Of Use
Main Page     |     City     |     Events     |     Map     |     Tourism     |     Help